25 Juni 2025 - 12:57
Source: ABNA
Khatibzadeh: "Amerika Imetuma Ujumbe Kwa Iran Kusitisha Vita"

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje ameeleza kuwa Washington ndiyo iliyotuma ujumbe kwa Iran wa kusitisha vita, akisisitiza kuwa Washington inapaswa kulipa fidia kwa uharibifu iliosababisha kwenye vituo vya Iran.

Saeed Khatibzadeh, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, katika mahojiano na Al Mayadeen, alitangaza: "Tehran ilisimama imara na kwa nguvu dhidi ya uchokozi wa Israel na ikastahimili. Uchokozi wowote utakaofanywa dhidi ya Iran, tutaujibu kwa nguvu na uthabiti."

Khatibzadeh alifafanua: "Tulishambulia kituo kimoja kilichokuwa chini ya udhibiti wa Amerika. Tuko tayari kujibu uchokozi wowote na Washington ndiyo iliyotutumia ujumbe wa kusitisha vita."

Aliongeza: "Wakazi wa maeneo yanayokaliwa wanapaswa kujua kwamba wao ni waathirika wa makosa ya kimkakati ya Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni."

Khatibzadeh alisema: "Iran imedhamiria kupinga na utawala wa Kizayuni umepigwa kofi kali."

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran aliendelea: "Washington inapaswa kulipa fidia kwa uharibifu iliosababisha kwenye vituo vya Iran, na tutawasilisha malalamiko katika Umoja wa Mataifa."

Saeed Khatibzadeh katika mahojiano na Al Mayadeen alisema: "Huwezi kulipua sayansi na uwezo wa kiufundi na teknolojia nchini Iran."

Alibainisha: "Iran ni ustaarabu na haiwezi kuharibiwa, na Rais wa Amerika anapaswa kujua hili."

Khatibzadeh alisema: "Iran imetangaza waziwazi kuwa uchokozi uliotokea umeharibu kanuni ya diplomasia na Iran haimwamini mpatanishi aliyepanga njama dhidi yetu. Kile ambacho hakikufikiwa kwa uchokozi, hakitafikiwa pia kwa diplomasia."

Alisisitiza: "Rafael Grossi anapaswa kuwajibika baada ya kutekeleza jukumu la kusikitisha kwa kuandaa njia ya makabiliano."

Your Comment

You are replying to: .
captcha